Lissu asherehekea 'Birthday' ya Maalim Seif kisiwani Pemba
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu, hii leo aliungana na mgombea urais wa Zanzibar kupitia ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, kwenye sherehe za kuzaliwa kwa Maalim Seif anayetimiza miaka 77. Sherehe hizo fupi kwenye Viwanja vya Tibirinzi zilikuwa sehemu ya ufungaji wa kampeni za Maalim Seif kisiwani Pemba.